Genesis 9:23-26

23Lakini Shemu na Yafethi wakachukua nguo wakaitanda mabegani mwao wote wawili, kisha wakaenda kinyumenyume, wakaufunika uchi wa baba yao. Nyuso zao zilielekea upande mwingine ili wasiuone uchi wa baba yao.

24Nuhu alipolevuka kutoka kwenye mvinyo wake na kujua lile ambalo mwanawe mdogo kuliko wote alilokuwa amemtendea, 25 aakasema, “Alaaniwe Kanaani!
Atakuwa mtumwa wa chini sana
kuliko watumwa wote kwa ndugu zake.”

26 bPia akasema, “Abarikiwe Bwana, Mungu wa Shemu!
Kanaani na awe mtumwa wa Shemu.
Copyright information for SwhKC